HISTORIA YA VITA BARIDI AMBAYO INAENDELEA KWA SASA KATI YA RUSSIA NA MATAIFA MENGINE
Vita baridi ilikuwa
kipindi cha ugomvi kati ya vikundi viwili vya nchi duniani kati ya 1945 na
1989. Upande moja zilikuwa nchi zilizoshikama na Marekani ya Ulaya ya Magharibi katika NATO
na upande mwingine nchi zilizoshikamana na Umoja wa Kisovyeti
na madola ya Ulaya ya Mashariki.
Vita baridi badala ya vita moto
Pande zote
mbili zilijenga jeshi kubwa na kuwa na silaha nyingi lakini hazikuanzisha vita
moja kwa moja ingawa zilijaribu kutishana na kupeana matatizo kwa njia nyingi.
Kipindi hiki kilikuwa na maandilizi ya vita lakini vita ya kijeshi haikuanza.
Sababu muhimu ya kutoingia katika mapigano ya wazi ilikuwa akiba kubwa ya silaha
za nyuklia kila upande na wote walijua ya kwamba vita ingeleta uharibifu kabisa
kwa nchi zote zilizoshiriki hata kwa dunia yote.WWW.PALLANGYO.BLOGSPOT.COM
Chanzo kilikuwa farakano kati ya washindi wa Vita Kuu ya
Pili ya Dunia
Vita baridi
ilianza baada ya vita kuu ya pili ya
dunia. Marekani, Umoja wa Kisovyeti, Uingereza na Ufaransa zilikuwa nchi washindi wa vita hii dhidi
ya Ujerumani. Urusi ulikuwa na siasa ya kikomunisti lakini washindi wengine
walifuata siasa ya kidemokrasia pamoja na uchumi wa kibepari.
Nchi za Ulaya
ya Mashariki pamoja na sehemu za Ulaya ya Kati zilikaliwa na jeshi la kisovyeti
lililowahi kuwafukuza Wajerumani katika maeneno haya. Wasovyeti walianza kuunda
serikali zilizoshikamana nao mara nyingi kwa njia ya uchaguzi bandia na kwa
kuwalazimisha wanasiasa wa nchi kama Poland, Chekoslovakia au Hungaria kutii madai yao. Wapinzani walikamatwa
na kufungwa ndani. Katika kila nchi chama cha kikomunisti kiliingizwa katika
serikali na vyama vingine vya kisiasa kuwekwa chini ya usimamizi wa wakomunisti
au washauri wasovyeti. Mwaka 1946 kiongozi Mwingereza Winston Churchill alilalamika ya kwamba
"pazia ya chuma" ilitandikwa katika Ulaya kuanzia Stettin
upande wa kaskazini hadi Trieste upande wa kusini na
nyuma yake uhuru ulikandamizwa.
Viongozi wa
nchi za magharibi waliona maendeleo yale kama tishio hata kwa nchi zao ambako
vyama vya kikomunisti vililenga pia kushika utawala lakini kwa jumla
zilishindwa bila usaidizi wa kijeshi jinsi ilivyokuwa upande wa mashariki. Hapa
nchi za Ulaya ya Madharibi zilishikamana pamoja kuzuia uenezaji wa enzi la
Kisovyeti katika nchi zao.
Uhusiano mbaya
ulianza mara baada ya ushindi ukaonekana kabisa wakati wa 1948/49 ambako
Wasovyeti walijaribu kuwalazimisha Wamarekani na wanzao kuondoka katika Berlin
ya Magharibi kwa kufunga barabara zote zlizounganisha mji na
Ujerumani ya Magharibi na kuzuia vyakula visifike mjini tena. Marekani iliweza
kulisha wakazi kwa njia ya daraja la
angani na ndege zilileta bidhaa.
Kabla ya tukio
hili majaribio la Umoja wa Kisovyeti la kupanusha upeo wake kwa kusaidia wanamigambo
wakomunisti katika Ugiriki na Uajemi kuanzia 1946 yalileta uchungu. Sababu nyingine za
kuunda wasiwasi zilikuwa majaribio ya wapelelezi Warusi waliotafuta siri ya silaha
za kinyuklia za Marekani.
Ukuta wa Berlin
ilikuwa kielelezo wa pazia ya chuma katika Ulaya
NATO na Mapatano ya Warshawa
Nchi za
Magharibi ziliunda mwungano wa kijeshi wa NATO
(North Atlantic Treaty Organization) wakiahidi kushikamana kama nchi yoyote
ingeshambuliwa na nje.
Wasovyeti
walijibu kwa kuunganisha nchi zilizokuwa chini ya usimamizi wao katika Mapatano ya Warshawa.
Miungano haya
ya kijeshi yalifuatwa na mapatano ya kiuchumi kila upande.
Nchi
zilizoanzisha NATO zilikuwa: Marekani, Uingereza, Ufaransa, Italia, Ureno,
Uholanzi, Ubelgiji, Luxemburg, Norwei, Denmark, Iceland, Australia na Kanada.
1954 Ujerumani
ya Magharibi ilipokelewa pia. Uturuki na Ugiriki zilijiunga pia.
Nchi za
Mapatano ya Warshawa zilikuwa: Umoja wa Kisoveti, Albania, Bulgaria, Poland, Romania, Chekoslovakia, Hungaria na Ujerumani
ya Mashariki.
Kila upande
ulikuwa na nchi mbalimbali zilizoshirikiana nao bila kijiunga rasmi na mapatano
yale. Umoja wa Kisoveti ilishikamana na Kuba,
China, Korea ya Kaskazini
na Mongolia. Marekani iliendelea kuwa na mapatano ya
kijeshi na nchi nyingi kama Uajemi, Pakistan na Taiwan.
Makombora
maelfu kama SS20 hii ya kisovyeti yalikuwa tayari kurusha mabomu ya kinyuklia
Tishio la vita ya nyuklia
1945 Marekani
ilikuwa nchi ya pekee duniani yenye silaha za nyuklia. Lakini Umoja wa
Kisovyeti iliweza kufuata 1949 ikalipusha bomu ya nyuklia.
Kila upande
uliendelea kutengeneza akiba kubwa ya silaha hizi. Hadi miaka ya 1980 idadi ya
silaha hizi ilitosha kuharibu kila maisha duniani mara kadhaa.
Viongozi wa
kijeshi na wa siasa walijua ya kwamba kama ulikuwa na uwezo wa kuharibu kabisa
maadui. Lakini walijua pia ya kwamba hata maadui wale walikuwa na uwezo huohuo
na kila moja aliyjiandaa kabisa kurusha mabomu nyingi kabla ya kufa mwenyewe.
Kwa njia hii
hofu ya kifo cha kinyuklia ilizuia kuanzishwa kwa vita moto kati ya pande
mbili.
Lakini hofu hii
haikuzuia vita katika nchi mbalimbali ambako Wasovyeti na Marekani walisaidia
upande moja dhidi ya marafiki wa upande mwingine. Mifano ya vita hizi ni Vita ya Korea na Vita ya Vietnam au pia vita katika Afrika.
Athira ya vita
baridi duniani mnamo mwaka 1980
Buluu neusi: Nchi za NATO
Buluu nyeupe:Nchi zilikuwa na mapatano ya kijeshi na Marekani
Nyekundu kali: Nchi za mapatano ya Warshawa
Nyekundu wastani: Nchi za kisoshalisti zenye makubaliano nao
Nyekundu nyeupe:Mchi zenye mapatanao mengine na Umoja wa Kisovyeti;
Kijivu: Nchi zisizofungamana na upande wowote
Buluu neusi: Nchi za NATO
Buluu nyeupe:Nchi zilikuwa na mapatano ya kijeshi na Marekani
Nyekundu kali: Nchi za mapatano ya Warshawa
Nyekundu wastani: Nchi za kisoshalisti zenye makubaliano nao
Nyekundu nyeupe:Mchi zenye mapatanao mengine na Umoja wa Kisovyeti;
Kijivu: Nchi zisizofungamana na upande wowote
Athira ya vita baridi katika Afrika
Maendeleo ya
Afrika yaliathiriwa pia na vita baridi. Kwa jumla kila upande ulijaribu kuvuta
nchi changa za Afrika upande wao. Kama serikali ilipatana na upande mmoja
upande mwingine mara nyingi ulikuwa tayari kusaidia wapinzani wa ndani kwa
msaada wa silaha na pesa.
Wapiganaji
uhuru katika koloni za Ureno kama Msumbiji au Angola walipata msaada wa silaha na pesa kutoka nchi za
mashariki kwa sababu Ureno ilikuwa nchi ya NATO. Wapinzani hao walitazamiwa na
magharibi kama wakomunisti na wakala wa Wasovyeti hivyo Marekani ilisaidia
Afrika Kusini ingawa siasa ya ubaguzi wa rangi ilivunja haki za kidemokrasia.
Madikteta wengi
wa Afrika walipata usaidizi wa upande mmoja au mwingine wakitangaza tu
kushikamana nao. Serikali ya Mobutu Sese Seko katika Kongo ilisaidiwa na nchi
za magharibi kwa sababu Mobutu alijitangaza kama adui wa ukomunisti. Haile
Mengistu Mariam wa Ethiopia alipata silaha na
washauri kutoka upande wa mashariki na polisi ya siri ya Ujerumani ya Mashariki
ilishauri wapelelezi wa Ethiopia jinsi gani kutafuta wapinzani wa ndani. Hata
kama serikali fulani ya Afrika iliharibu uchumi na kuvunja haki za binadamu
iliweza kutegemea usaidizi kutoka kwa upande moja wa vita baridi ikijitangaza
iko upande wao. Siad Barre alikuwa na mapatano na Umoja wa Kisovyeti hivyo
Somalia ilihesabiwa kati ya nchi za upande wa kikomunisti. Baada ya Ethiopia
kupatana na Wasovyeti pia tangu 1974 Somalia iliyokuwa na fitina na jirani yake
kuhusu eneo la Ogaden ilihamia upande wa Marekani ikasaidiwa
nao.
Viongozi
mbalimbali waliopigania uhuru walipata kimbilio katika nchi za mashariki
wakapata nafasi ya kusoma na kujifunza matumizi ya silaha. Hii ilikuwa sababu
moja kwa nini wengi walielekea itikadi ya kisoshalisti na kujaribu mbinu za
kisiasa na kiuchumi kufuatana mfano wa wakomunisti wa Ulaya hata kama siasa yao
haikuwa na matokeo mazuri kwao nyumbani.
Mwisho 1989
Mashindano ya
kuongeza silaha mpya yalishinda uwezo wa uchumi wa nchi za kikomunisti. Katika
miaka ya 1970 ilionekana ya kwamba uchumi wao ulibaki nyuma. Teknolojia mpya
hazikuenea kwa sababu utawala wa kidikteta ulijaribu kusimamia mawasilaino yote
kwa njia ya polisi na manedleo yalikwama. Uchumi ulioongozwa na serikali
haukuweza kushindana na nguvu ya ubepari.
Umoja wa
Kisovyeti ilitia nguvu jeshi na maendeleo ya silaha lakini uwezo wa kiuchumi
haukutosha.
Katika miaka ya
1980 ilionekana ya kwamba nchi za mashariki zilibaki nyuma sana. Katika nchi
kadhaa wananchi walidai haki za kibinadamu. Poland iliona harakati ya
wafanyakazi waliokataa uongozi wa wakomunisti wakaanzisha chama cha Solidarnocz
na kusababisha utawala wa kijeshi badala ya chama.
Michael
Gorbachov wa Umoja wa Kisovyeti na rais Ronald Reagan wa Marekani wakitia
sahihi mapatanoy a kupunguza silaha za kinyuklia 1997
Kiongozi mpya
wa Umoja wa Kisovyeti Mikhail
Gorbachov alielewa hatari ya kuporomoka kwa uchumi wake akatafuta
uelewano na Marekani ili kupunguza gharama za jeshi. Siasa mpya ya glasnost
iliruhusu kutamka kwa maoni mbalimbali ikaruhusu pia kiwango fulani cha
upinzani wa viongozi. Gorbachov aliamua kutotisha tena nchi zilizoshikamana na
Umoja wa Kisovyeti kwa mashambulio ya kijeshi jinsi ilivyokuwa awali.
Hapo nguvu za
upinzani zilipata kipaumbele katika nchi kama Hungaria na Poland na viongozi
wapya walielekea kuongeza haki za kidemokrasia wakakubali vyama vipya na
magazeti huru. Mwaka 1989 wananchi wa Ujerumani ya Mashariki walianza
kuandamana wakalazimisha uongozi wa chama cha kikomunisti kujiuzulu na viongozi
wapya walifungua ukuta wa Berlin
iliyowahi kutenganisha pande mbili za mji huu kwa miaka 38.
Anguko la
ukuita wa Berlin ilikuwa dalili ya mwisho wa vita baridi na pia utawala wa
kikomunisti katika nchi za Ulaya. Kote katika nchi za kikomunistis erikali
ilianguka na viongozi wapya walichaguiwa na wananachi.



