Martinez: Asema kilichomvutia kumsajili Samuel Eto'o kwa miaka miwili
Mshambuliaji kutoka nyumbani Afrika katika nchi ya Cameroon
Samuel Eto'o Fils ametambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari ikiwa ni
siku moja baada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Everton
kwa mkataba wa miaka miwili.
Meneja wa klabu ya Everton Roberto MartÃnez Montoliú amemtambulisha Eto’o mbele ya waandishi wa habari pamoja na kutoa sababu za kile kilichomvutia kumsajili mshambuliaji huyo ambaye msimu uliopita aliitumikia Chelsea kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Martinez amesema uwajibikaji na kujituma kwa mshambuliaji huyo kutoka nyumbani Afrika ndio chagizo kubwa lililompa msukumo wa kumsajili baada ya kuona uwezekano wa kuwa nae kwenye kikosi cha The Toffees.
Amesema kabla ya kukamilisha mipango ya kumsaili aliketi kitini na Samuel Eto’o na kumueleza nini anachokihitaji kutoka kwake na mwishowe walifikia makubaliano ya kiutendaji, hali ambayo anaamini aitakamilishwa kwa vitendo uwanjani.
Samuel Eto’o anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Everton ambacho mwishoni mwa juma hili kitapambana na Chelsea kwenye uwanja wa Goodson Park huko jijini Liverpool.