Andy Murray: Sijutii Kuunga Mkono Harakati Za Uhuru Wa Scottland

Shirikisho la mchezo wa Tennis nchini Uingereza, limesema kuwa Andy Murray ni mzalendo kwa nchi ya hiyo baada ya kukosolewa kwa kuunga mkono uhuru wa Scottland.

Murray, alikosolewa kwenye mitandao ya kijamii, baada ya kuandika kwenye mtandao wa tweeter kuwa anaungana na wale wanaosema Ndio..kwa maana ya wanaounga mkono Scottland kupata uhuru wake.
Mkurugenzi mtendaji wa shirikisho la mchezo wa Tennis nchini Uingereza, Michael Downey amesema anamuunga mkono Murray kwa kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia na alikuwa ana haki ya kutoa maoni yake kwa ajili ya mustakabali wa nchi yake.
Kwa upande wa Murray amesema katu hatojutia maamuzi ya kuungana wananchi ya Scotland waliokuwa wanataka kuona nchi yao inapata uhuru.

Popular Posts