Joey Barton Aibua Mapya Kwa Balotelli
Wakati sakata la kubaguli kwa mshambuliaji kutoka nchini
Italia na klabu ya Liverpool, Super Mario Barwuah Balotelli kupitia
mtandao wa kijamii wa Twitter likiendelea kufukuta, usiku wa hii leo
kiungo wa klabu ya Queens Park Rangers, Joseph Anthony Joey Barton
ametoka na jipya.
Barton, ambaye anasifika kwa sifa ya utukutu amemshambulia wazi wazi Balotelli kupitia mtandao wa Twitter kwa kumfananisha na mzimu ambao haujielewi katika tasnia ya soka duniani.
Barton, aliweka ujumbe kupitia akaunti yake ya Twitter wakati mchezo wa kombe la ligi ukiendelea kati ya Liverpool dhidi ya Middlesborough katika uwanja wa Anfield.
Katika ujumbe huo wa Barton, umesomeka kwamba Balotelli hawezi kuwa sehemu ya kuziba nafasi iliyoachwa na mshambuliaji kutoka nchini Uruguay Luis Alberto Suarez Diaz aliyetimkia FC Barcelona na badala yake amekuwa akihangaika kama mzimu usiojielewa uwanjani.
Tayari imeanza kuhisiwa huenda Barton akajikuta akiingia kwenye matatizo makubwa kwa kujumuishwa na wadau wa soka waliomtusi na kumbagua Balotelli mwishoni mwa juma lililopita kupitia mtandao wa Twitter baada ya kuchukizwa na ujumbe uliowekwa na mshambuliaji huyo kuhusu kufungwa kwa Man Utd mabao matano kwa matatu dhidi ya Leicester City mwishoni mwa juma lililopita.
Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa Joey Barton kumchokonoa Balotelli, kwani aliwahi kujaribu kupigana nae uwanjani wakati akiwa na klabu ya Man City mwaka 2012 na mwishowe wote wawili waliadhibiwa na muamuzi kwa kuonyeshwa kadi nyekundu.