kesi ya kumpiga Rihanna ni kama bado inamtia gundu Chris Brown

Chris Brown ni kama huu mwaka haujaanza poa kwake, katika vitu ambavyo amekutana navyo ni vikwazo kwenye kazi yake ya muziki siku ya January 02 mwaka huu nilikuandikia story ya staa huyo

 kushindwa kwenda kupiga show yake Ufilipino baada ya kupoteza passport muda mfupi kabla ya safari, wiki chache mbele akashindwa pia kuanza tour yake yaBetween the Sheets baada ya Mahakama kumzuia ili amalizie saa 100 za adhabu ya kufanya kazi za kijamii kutokana na kesi ya kumpiga Rihanna ambayo imeendelea kuwepo Mahakamani kwa zaidi ya miaka mitano.
Leo kuna story ambayo iko kwenye headlines kuhusu yeye tena, amezuiwa kuingia Canada kufanya show kubwa ambayo ilikuwa ifanyike siku ya leo February 25, sababu haijafahamika lakini ishu ya kesi yake hiyo inatajwa kwamba huenda imemtia doa kutokana na Sheria za nchi nyingi Duniani kutoruhusu mtu ambaye ana rekodi za uhalifu kuingia ndani ya nchi zao.
chris-brown-600
Chris akiwa Mahakamani siku za nyuma
Chris aliandika kwenye ukurasa wake Twitter kwamba anasikitika kuikosa show hiyo; “The good people of the Canadian government wouldn’t allow me entry. I’ll be back this summer and will hopefully see all my Canadian fans!”—Tweet ambayo muda mfupi baadaye aliifuta.
Jamaa ambao waliandaa show hiyo wamesema wanafanya utaratibu ili kupata kibali cha kumruhusu Chris kuingia Canada ili amalizane na ‘deni’ la kutoa burudani kwa fans wake, japo wamesema kwa wale ambao wameshanunua ticket wanaweza kurudishiwa pesa zao kwenye vituo walikouziwa ticket hizo.

Popular Posts