LHRC yalaani kitendo cha baadhi ya wabunge kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge.


Kituo cha sheria na haki za binadamu kimelaani vikali kitendo cha baadhi ya wabunge kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge na kulitaka bunge kuwarudisha kwani kwa kufanya hivyo ni kuwakosesha wananchi haki yao ya uwakilishi katika chombo hicho
muhimu sambamba na kuitaka serikali isitishe uamuzi wake wa kuwafukuza wanafunzi wa UDOM.
Akitoa tamko hilo mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho Dk Hellen Kijo Bisimba amesema wabunge hao wamesimamishwa wakati walikuwa wakiwatetea wananchi wao.
 
Evansi Sichalwe na Geline Fuko ni wanasheria ambao wanasema wananchi walikuwa na matumaini makubwa na bunge la sasa na ukizungatia kuwa limepata spika ambaye alikuiwa naibu spika katika bunge la tisa na hivyo walitegemea lingeongozwa kwa umahiri mkubwa   lakini kanuni na sheria nyingi zinakanyagwa kila kukicha.
 
Badhi ya wananchi kutoka katika maeneo mbalimbali ya jiji wamekuwa na mitizamo yao tofauti tofauti wengie wakishauri busara zitumike katika kupata ufumbuzi na wengine wakisema lazika kanuni zilizowekwa ndio zitumike kuendesha bunge hilo.

chanzo itv

Popular Posts