JE? NDEGE YA MALAYSIA IKO HAPA???? ALIENS WAKO NAYO??? BAHARI YA SHETANI???SOMA HII RIPOTI
Bermuda Triangle ni eneo la pembe tatu la bahari lililopo
kati ya nchi tatu katika bahari ya Atlantiki.Miji hiyo ni Bermuda,Puerto Rico
na Fort Lauderdale.Meli,watu na ndege mbalimbali zimeripotiwa kupotea
kutokuonekana milele katika eneo la Bermuda Triangle.Muda mfupi eneo hili
limekuwa likipata umaarufu na kupewa jina la Devil's sea (Bahari ya Shetani)
ambapo
binadamu wamekuwa wakiamini au kujenga imani potofu za kishirikina kuwa
shetani amekuwa na makazi katika eneo hilo na kuwapoteza wasafiri wa majini ikiwa
ni pamoja na vyombo vyao vya usafiri,lakini uhalisia katika eno hili la maji
mafupi ni ukweli kuhusu shetani? au Aliens wamekuwa wakitumia eneo hili kama
kituo chao katika dunia.Inawezekana kuna ukweli juu ya swala la kina hiki
kuwameza watu katika eneo hili.
Historia
ya eneo hili imekuja kuzuka katika chombo cha habari cha Associated Press
dispatch cha Septemba 16,1950.Mwana habari E.V.M Jones aliandika kuhusu
upoteaji wa ajabu wa meli na ndege
katikati ya pwani ya Florida na Bermuda.Miaka miwili baadae kipengele
kilionekana katika jarida ikiwa na kipengele kingine kilicho andikwa na George
X. Sand kuhusu "Mtiririko wa kutisha wa upoteaji wa vyombo vya
majini" ambao umechukua nafasi katika miaka kadhaa iliyopita.
Ulipita
muda mrefu kabla ya mawazo na mitazamo iliyotolewakuhusu kipande hiki cha
bahari. M.K Jessup aliandika kuhusu upoteaji na akatoa mawazo kuhusu upeo
mkubwa wa kiakili wa Aliens ( Viumbe wa Ajabu ) kuhusiana na swala hili katika
kitabu cha "The Case for the UFO". Urejeo wa kitabu hicho ulikuja
kutolewa na Donald E. Kyhoe wa kitabu cha "The Flying Saucer
Conspiracy" cha 1955.Frank Edwards wa "Stranger Than Science"
alikuja kukubaliana na wazokuhusu Aliens kwa kuwa na makazi katika eneo hilo la
pembe tatu pia.Mwishoni Vincent H. Gaddis alikuja na ripoti kuhusu
"Bermuda Tringle".Huyu aliandika kipengele katikamwezi wa Februari ya
mwaka 1964 ambapo baadae alikuja kuandika historia katika kitabu chake
"Ivisible Horizons" iliyoitwa "The Deadly Bermuda
Triangle".
Mika mingi imepita na vipengele,vitabu,mtiririko wa vipindi vya
televisheni na filamu mbalimbali zimetengenezwa kuhusu kitu hiki cha
kushangaza,lakini mtu yeyote mwenye mawazo juu ya swala hili lazima atajiuliza
juu ya kwanini meli,ndege na watu wamekuwa wakipotelea katika kipande hiki cha
bahari? Je,hawaogopi kusafiri?
Moja ya
historia maarufu katika eneo la Bermuda Triangle juu ya kupotea kwa kushangaza
ni ya ndege ya Air Flight 19.Je,nini kilitokea?
Desemba 5
ya mwaka 1945,ndege ya mabomu iliondoka katika kituo cha kijeshi cha ndege
katika ngome ya Lauderdale na hawakurudi.Ndege hii ilikuwa na watu 14 ambao 13
miongoni mwao walikuwa ni wanafunzi wa urubani katika hatua ya mwisho ya
mafunzo wakiwa na Luteni Charles Taylor.Marubani wengine watano walikuwa tayari
wamekwisha kusafirishwa kutoka katika kituo cha Miami cha ndege.Luteni Taylor
alikuwa tayari na uelewa mzuri wa eneo la Florida ingawa hakuwa na uelewa wa
kusafiri angani katika eneo la Bahamas ambapo ndio ndege ya Flight 19 ilitakiwa
kuelekea.
Wazo lao
kwa siku ile ilkuwa ni mazoezi ya kulipua mabomu katika eneo la kufugia kuku
maili 56 kutoka katika kituo cha kijeshi cha ndege katika ngome ya
Lauderdale.Swala hilo kwa mara moja lilifanikiwa.Marubani hao walitakiwa
kundelea kuelekea upande wa mashariki kwa maili 67 na baadae kuelekea kaskazini
kwa maili 73.Baadae walitakiwa kurudi kusini magharibi kuelekea nyumbani yaani
katika eneo waliloanzia safari.Kwa maneno mengine walikuwa wakisafiri safari ya
njia ya pembe tatu ambayo iliitwa Bermuda Tringle.
Muda wa
saa 9:50 mchana,rubani na waelekezaji wa ndege ile,Luteni Robert Cox walikuwa
karibu kutua katika ngome ya Lauderdale.Walisikia sauti ya mtu aliyeitwa Powers
kupitia mawimbi ya redio.Powers akajibu "Sijui hapa tulipo ni wapi ,lazima
tutakuwa tumepotea baada ya kugeuka kwa mara ya mwisho".
Baada ya
muda mfupi ,Luteni Cox aliweza kugundua sauti kupitia mawasiliano ya radio na
rubani mwingine wa wasafiri waliopotea katika bahari wakiongea na Luteni
Taylor.Alitaarifiwa kuwa dira za Taylor zilikuwa hazifanyi kazi tena na hivyo
walikuwa na uhakika kuwa walikuwa katika eneo la karibu,yaani la Florida,ingawa
hakujua jinsi ya kufika katika eneo au ngome ya Lauderdale.
Tangu
hapo mawasiliano yakawa yamekatika kati ya kituo cha Lauderdale na ndege ya
wanafunzi wa urubani ya Flight 19.Hii ilichangiwa na hali ya hewa ya anga yaani
Atmospheric Condition kwa lugha ya kitaalamu ambayo ilichangia katika ukatikaji
wa mawasiliano ya mawimbi ya radio.Mpaka kufikia muda wa saa 11:15 ya
jioni,ndege ya Taylor ilikuwa bado haijatua katika kiwanja changome ya
Lauderdale.
Baada ya
kuona mawasiliano yamekosekana,Luteni Taylor aliamua kuendelea na mafunzo na
wanafunzi wake kuelekea kaskazini.Ndege ya uokoaji iltumwa muda wa saa 12:20
jioni.Ilikuwa ni ndege yenye uwezo wa kupaa na kusafiri kwenye maji kama
meli.Muda mfupi baadae ilipoteza mawasiliano jambo ambalo lilileta wasiwasi
miongoni mwa wahusika wa kambi hiyo ya ngome ya Lauderdale.ndani ya saa
nzima,ndege nyingine zaidi zilirushwa ili kusaidia katika utafiti huo.Kwa kweli
hali ya hewa ilikuwa mbaya na bahari iliripotiwa kuchafuka kwa hali ya hatari
zaidi.Ndege moja tena ya Martin Mariner ( Training 49 ) ilishindwa kutoa majibu
katika mawimbi ya radio.
Muda wa
saa 1:50 usiku,radio za meli moja iliyokuwa baarini zilitoa taarifa kuhusu
kuonekana kwa moto mkubwa uliosababishwa na mlipuko wa ndege.Meli hiyo ilieleza
kuwa baadaye palionekana kiasi kikubwa cha mafuta yakisambaa baharini na
hapakupatikana mwili wowote wa majeruhi ya wa tu katika ndege hiyo
iliyolipuka.Kwa kweli walishindwa kupata mafanikio yeyote kutokana na hali ya
hewa kuwa mbaya na ya kutisha.
Ndege
hiyo ya Flight 19 kwa muda huo ilikuwa imeishiwa kabisa mafuta na ilianza
kuteremka kuelekea aridhini.Mawasiliano ya mwisho na Taylor yalisikika muda wa
saa1;04 za jioni.Utafutaji wa marubani hao waliopotea uliendelea usiku kucha na
siku iliyofuata mamia ya ndege na meli ziliongezeka katika shughuli hiyo.
Kwa
kweli hapakupatikana rubani wowote wale.
Aprili
3,1946 lilitolewa hitimisho ambalo lileta utata miongoni mwa ndugu wa marubani waliopotea wakiwamo mama mzazi wa
Taylor na mama mdogo ambao walishindwa kabisa kukubaliana na maelezo
yaliyotolewa kuhusiana na tukio hilo.
Upoteaji
wa marubani hao ulileta mkanganyiko wa hali ya juu kuhusiana na Je,inawezekana
vipi kwa vyombo vikubwa kama vile kuzama katika bahari fupi na kushindwa
kuonekana muda wote na mahali popote pale?
Makosa
na taarifa zisizoeleweka kuhusu upoteaji wa mwanamaji na ndege ya Flight 19
muda mfupi zilianza mapema katika miaka ya hamsini.historia mbalimbali kuhusu
sehemu ya kushangaza na ya kustaajabisha ambayo meli kubwa na ndogo na ndege
zimepotelea hapo na "limbo of the lost" imekamata sana akili za watu
kwa ghafla,gwiji lia pembe tatu ya Bermuda ilianza na bado inaendelea
kuwashangaza watu mpaka leo hii.
Taylor
alikaririwa akiongea katika mawimbi ya radio akisema "Kila kitu hakiko
sawa......inashangaza.....bahari haionekani kama ambavyo ilitakiwa kuwa"
na "Wanaonekana kama wanatoka anga la mbali-usinitafute".Haya ni
maneno ambayo yalizungumzwa na Taylor kabla ya kukata mawasiliano.Hii
inapelekea kuwepo histori ya aliens katika swala la uzamishaji wa meli katika
eneo la pembe tatu hilo.Hata katika move ya "Close Encounters of the Third
Kind" Steven Speilberg nyaraka za Flight 19 zinakumbusha juu ya chombo
kikubwa cha angani.Pia inaripotiwa kuwa katika siku ambayo upoteaji wa Flight
19 ulitokea,bahari ilikuwa tulivu.Kiukweli walikuwa wakijichanganya sana bila
ya kuelewa ni nini kilitokea kwa siku ile.
Mwaka
1991,gqzeti la habari liliandika taarifa yenye kichwa cha habari "Deep
Sea" kuhusu kuonekana au kupatikana kwa mabaki ya Flight 19 katika kina cha bahari maili kumi kaskazini
mashariki kutoka katika ngome ya Lauderdale.Ndege moja yenye nambari 28,sawa na
ile ya Taylor.Lakini mwezi Juni Graham Hawkes,ambaye aliongoza utafiti alisema kwamba
matokeo ya utafiti wa ziada hayaoneshi kuwa mabaki yaliyopatikana hayawiani na
yale ya Flight 19,hata namba za ndege hiyo hazikuwepo katika Flight 19.Pia
ndege hiyo ilipata ajali muda mrefu uliopita kabla ya Flight 19 kupotea.
Ukweli ni
kwamba kumekuwa na historia mbalimbali za kustaajabisha watu kuhusu upoteaji wa
meli na ndege aidha sehemu nyingine mbali na Eneo hilo la Bermuda ama ndani ya
sehemu yenyewe.Ukweli ni nusu ya upoteaji
wa vyombo hivyo vya usafiri umetokea sehemu nyingine mbali kabisa na
Bermuda Triangle ingawa historia inaunganishwa na eneo la Bermda,au eneo hilo
la pembe tatu linaweza kuwa na nguvu ya kimaajabu inayoweza kusambaa sehemu
mbalimbali za bahari na kuzizamisha meli na ndege.
Ukweli ni
kwamba ajali zinatokea kutokana na sababu moja ama nyingine,ndege zinagongana
au kujigonga,meli zinazama.....hebu jaribu kuvuta kumbukumbu kwa
Titanic,iliaminika kutokuweza kuzama kwa kipindi kile.Utafiti wa Larry Kusche
unafafanua kuhusiana na taarifa zisizo za kweli kuhusiana na eneo lile.Baada ya
kufanya utafiti bila ya kuchoka kupitia makala mbalimbali za magazeti,ripoti za
hali ya hewa na nyaraka za kiofisi,Kusche alipata taarifa kama alivyohisi
kwamba Bermuda Triangle haikuwa na upoteaji wowote kuliko sehemu yeyote katika
dunia hii.Ana kitabu kiitwacho "The Bermuda Triangle Mystery".Tafuta
ujisomee.
Kijana panua ubongo wako kupitia elimu.Penda kusoma katika maisha yako.
