KUHUSU YULE MWANAJESHI ALIEWAPIGA RISASI WENZIE LEO
Wanajeshi wanne wamepigwa risasi na kuuawa katika kambi ya jeshi huko
Fort Hood jimboni Texas.Jenerali Mark Milley, amesema mwanajeshi mmoja ndiye aliyewafyetulia wenzake risasi hizo karibu na zahanati ya afya ya kijeshi ya Carl R Darnall iliyoko katika kambi hiyo ya Jeshi.
Watu watatu walifariki kabla ya mwanajeshi huyo kujipiga risasi na kujiua.
Wanajeshi wapato wanne wanatibiwa majeraha mabaya ya risasi.
Daktari mkuu wa zahanati hiyo Dakta Glen Couchman anaelezea majeraha wanayotibu.
''Wote walikuwa na majereha mbalimbali ya risasi kwenye vifua shingo na tumbo''.
''ninajua kuwa mtangulizi wangu Leon Pannetta aliwahi kusema kuwa tukio kama hili mwaka wa 2009 litachungzwa .
Ni wazi lazima kuna kitu kinachoendelea ambacho hakifai.
Lazima tutatue shida hii .''
Rais Obama amehuzunishwa sana na tukio hilo ambalo anasema limetokea katika kambi ambayo inapaswa kuwa salama .
Obama
"Haiwezekani kuwa tukio sawa na lile lililotokea miaka mitano iliyopita litokee tena na tukose kujiuliza kunani . Tunafahamu kuwa jamaa na familia zilizoko Fort Hood zimejitolea kwaajili ya usalama wa taifa letu. Tunahuzunishwa sana kuwa tukio hili limerudiwa katika kambi hii"
Hii siyo mara ya kwanza kwa kituo hicho kikubwa cha majeshi ya Marekani Fort Hood kushuhudia ufyetulianaji wa risasi .
Mwaka 2009 wakati dakatari wa magonjwa ya kiakili wa jeshi la Marekani meja Nidal Hasan alipowapiga risasi na kuwaua watu kumi na watatu.
Rais Obama amesema anafuatilia yanayotukia katika kambi hiyo kwa makini.
CHANZO BBC SWAHILI