INAWEZEKANA HUYU JAMAA YUKO PEKE YAKE DUNIANI



Drug addict finds £75k bag of cash - and hands it in                                       Ni ngumu kidogo kuamini hasa kama uko katika hali ya umasikini ila ndio kweli imetokea huko California.
 Joe Cornell, 52 ambae yuko kwenye kituo maalum kwa ajili ya kuacha kutumia madawa ya kulevya maarufu kama REHAB, bwana huyo ambae mlo wa siku moja ni shida kwake katika pitapita zake
alibahatika kuokota begi la pesa lenye kiasi cha dola 12500 kwa hesesabu za haraka ni kama bilion 2 za tanzania, ambapo hakuna mtu yoyote aliemuona wakati akiziokota kwasababu pesa hizo zilidondoka kutoka kwenye gari maalum la kusafirisha pesa.

"niliokota begi nikaona mamiloni ya pesa, yani ilikuwa ni pesa tu , kichwani kwangu nilikuwa nawaza wema na ouvu kwa pamoja, nikawaza kuhusu mke wangu na jinsi anavyopenda niwe mtu mwema basi hapo nikapata jibu, nirudushe pesa za watu,.mke wangu alifurahi sana aliposikia nilichotenda"

Mr. Cornell,amefanya kitu sahihi alisema msemaji wa kampuni iliyopoteza pesa hizo(security firm Brinks).
Kwa kurudisha fadhila Joe Cornell,alipewa zawadi ya kama milioni 10 vilevile kituo cha rehab(Salvation Army) alichopo kimepewa kiasa hicho.
TIZAMA VIDEO YA TUKIO ZIMA HAPA
                                                   www.pallangyo.blogspot.com

Popular Posts