JAMANI MKUMBUKE KULIPA LAIKI 6 MNAZODAIWA(HATA WEWE UNADAIWA)
"Mheshimiwa Naibu Spika, ukiligawa Deni la Taifa kwa Idadi ya Watanzania millioni 45, kila Mtanzania atakuwa anadaiwa Tsh 600,000/= (Laki Sita).
Mheshimiwa Naibu Spika, Hesabu hizi zinatokana na Takwimu za Deni la Taifa zinazoonyesha wazi kwamba, mwezi June mwaka jana 2013, Deni hili la Taifa lilikuwa Tsh Trilioni 21.2, lakini hadi mwezi January mwaka huu 2014, Deni hilo limepaa kwa kasi ya ajabu mpaka Tsh Trillioni 29.4, ikiwa ni Ongezeko la Tsh Trilioni 8.2 kwa kipindi cha miezi Sita (6months) tu.
Takwimu na Taarifa mbalimbali zinaonyesha wazi kwamba, Fedha hizo zilikopwa kwa ajili ya kuendeshea Warsha, Semina, Safari, Mafunzo na Matengenezo ya Magari. Mheshimiwa Naibu Spika, Licha ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kuahidi kwa muda mrefu kufanya ukaguzi maalumu wa Deni la Taifa, hadi sasa taarifa yake haijawasilishwa.
Ni lini Taarifa hiyo ya
CAG Itawasilishwa hapa Bungeni ili kuwawezesha Wananchi kufahamu undani wa Deni hili la Taifa, kwani Jambo hili sio la Siri?. Nawasilisha.
SOURCE MH. TUNDU LISSU FACEBOOK PAGE
www.pallangyo.blogspot.com