KAMA UMEZOEA KUONA KWENYE MOVIE BASI HII IMETOKEA LIVE

Watu kadhaa wamejeruhiwa baada ya makundi ya waumini wa madhehebu ya Sikh wakiwa wamejihami kwa mapanga kushambuliana ndani ya hekalu nchini India.
Mapigano hayo yalitokea huku
maombi maalum yakifanyika kuadhimisha operesheni mbaya ya kijeshi iliyofanyika mwaka 1984.
 
Duru zinasema kuwa makabliano katika hekalu hilo linalosifika sana kama eneo takatifu zaidi kwa waumini wa Sikh, yalitokea kufuatia utata kuhusu nani engehutubia wa kwanza.
Inaarifiwa waumini walianza kupigania kipaza sauti ndiposa vurugu zikaanza.

Picha za ukanda wa Video zinonaonyesha wanaume wakikimbia na kutoroka kutoka dhehebu hilo baadhi wakiwa na mapanga tayari kwa vita.
Duru zinasema angalau watu watatu wamepelekwa hospitalini wakiwa na majeraha.

Serikali ya India inasema kuwa watu 400 na wanajeshi 87 waliuawa katika operesheni ya jeshi iliyofanyika kuwaondoa waumini wa Sikh waliokuwa wanapigania kujitenga mwaka 1984.
Mauaji yalifanyika katika hekalu hilo lijulikanalo kama Golden Temple.
 
Lakini wasikh wenyewe wanasema kuwa idadi ya waumini waliofariki ilifika watu 1,000.
Hii leo mamia ya Wasikh walikusanyika katika hekalu hilo kuwakumbuka wale waliofariki miaka 30 iliyopita , lakini sherehe za maadhimisho zilisambaratika na kugeuka fujo.

''Kwa mara nyingine, hekalu limekosewa heshima,'' alisema Prem Singh Chandumajra, msemaji wa chama tawala katika jimbo la Punjab.
 
Bwana Chandumajra alisema kuwa makabiliano katika Hekalu hilo, ni jambo la kukemewa na kuwa wakuu wa hekalu watawachukulia hatua wale waliohusika.http://pallangyo.blogspot.com/
SOURCE BBCSWAHILI

Popular Posts