TETESI ZA SOKA KATIKA MAGAZETI NA TOVUTI ZA ULAYA
hizi ni tetesi za usajili kabla ya ligi kuu ya england kuanza mapema baada ya kombe la dunia
Chelsea watajaribu kumsajili kiungo wa Barcelona Cesc Fabegas kuziba nafasi ya Frank Lampard (Daily Telegraph),
nyota wa zamani wa Liverpool Robbie Fowler amemsihi Brendan Rodgers kumsajili Fabregas (Daily Express),
Tottenham wanamuulizia beki wa Feyenoord Daryl Janmaat, ambaye anasakwa na Manchester United na Napoli (Daily Mail),
kipa wa Chelsea anayechezea Atlètico Madrid kwa mkopo, Thibaut Courtois amethibitisha kuwa amezungumza na Jose Mourinho kuhusu hatma yake Stamford Bridge (Daily Star),
Stoke wanatarajia kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Man U, Mame Biram Diouf kutoka Hannover (Daily Mail),
Manchester United, Arsenal na Tottenham watazidiwa kete na Real Madrid kumsajili Arturo Vidal kutoka Juventus (Daily Express),
Bayern Munich wameonesha dalili za kumtaka beki wa Man City Aleksander Kolarov, lakini wanakabiliwa na upinzani kutoka Roma na Juventus (Daily Mail),
Wolfsburg inayocheza Bundesliga nayo inataka kumsajili striker wa Chelsea Romelu Lukaku (Daily Express),
meneja wa Hull City Steve Bruce atakamilisha uhamisho wa pauni milioni 9.75 wa Ryan Bertrand kutoka Chelsea na kiungo wa Marseille Morgan Amalfitano wiki hii (Daily Star),
Arsenal, Newcastle na West Ham wameambiwa watalazimika kutoa pauni milioni 19 kama watataka kumsajili mshambuliaji wa Swansea Wilfried Bony (Daily Mirror),
Chelsea huenda wakalazimika kutoka pauni milioni 37 kumsajili beki wa kushoto wa Atlètico Madrid Luis Filipe kutokana na utata kwenye mfumo wa kodi nchini Hispania (AS),
Liverpool na Manchester United zinamfuatilia mshambuliaji wa Barcelona Alexis Sanchez (Daily Star).
SHARE tetesi hizi na wapenzi wa soka. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Adios!
SOURCE SALIM KIKEKE
www.pallangyo.blogspot.com