ARSENAL HAIKUWA NA HADHI YA KUMSAJI SUAREZ...SIO MANENO YANGU ALIESEMA NI HUYU HAPA
Klabu bingwa ya
FA Cup Arsenal ilikuwa ni
moja ya timu iliyokaribia kabisa kumsaini mshambuliaji huyo wa Uruguay
baada ya kutuma ofa ya £40 na senti moja, ofa ambayo ilikuwa imefikia
kiasi ambacho Liverpool walikiweka kwenye mkataba ikiwa timu yoyote
itahitaji kumsaini Suarez, hata hivyo uhamisho huo ulishindikana na
Suarez akabaki Liverpool.
Takribani miezi 12 imeshapita sasa tangu
uhamisho huo ushindikane na Suarez tayari ameshaenda FC Barcelona kwa
ada ya uhamisho wa £75, na kuondoka kwake Liverpool kumeacha majonzi
makubwa Anfield, huku nahodha wa klabu hiyo Steven Gerrard akikiri
kuhuzunishwa mno na kuondoka kwa Suarez.
Pamoja na kukiri kuhuzunishwa na kuhama kwa
Luis Suarez, Gerrard pia amezungumzia sakata la uhamisho wa Suarez
uliofeli kwenda Gunners.
Gerrard anasema: “Ningeumia zaidi na
kuhuzunishwa kumuona Luis akihamia Arsenal. Pamoja na heshima
nilizonayo kwa Arsenal, nilimwambia kwamba kwa kiwango chake kikubwa
hakustahili kuichezea Arsenal. Nilimwambia kama utaendelea kuwa nasi,
ukafunga mabao 30 basi utashinda uchezaji bora wa ligi pamoja na tuzo ya
mchezaji bora wa chama cha waandishi wa habari – na hapo ndipo Real au
Barcelona zitakufuata kukusajili. Nadhani watu wengine wa karibu
walimshauri vibaya msimu uliopita, wakimwambia anahitaji kucheza kwenye
champions league bila kujali kwenye timu gani.”
Nahodha huyo wa Liverpool aliendelea kusema
kwamba kama mshambuliaji huyo angeendelea kubaki Liverpool msimu huu,
basi klabu yao ingekuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa: “Naamini kama
tungekuwa na Suarez basi tungekuwa na nafasi zaidi. Nina majonzi kuona
ameondoka lakini nina furaha kwa ajili yake kwa sababu amepata
alichotaka na anachostahili.”