CHAMBERS RASMI ARSENAL


 
Arsenal wamemsajili mchezaji wa kimataifa wa England chini ya umri wa miaka 19 Calum Chambers kutoka Southampton kwa pauni milioni 16. Mchezaji huyo alicheza mechi 25 kwa Southampton msimu uliopita, na Arsenal wanamuona kama beki wa akiba wa kulia, au beki wa kati au hata kiungo. "Jinsi alivyoweza kuzoea kucheza ligi ya England msimu uliopita katika umri mdogo, inaonesha ana ubora wa hali ya juu," amesema Arsene Wenger. Arsenal pia wamemuulizia kiungo wa Southampton, Morgan Schneiderlin, 24.


Popular Posts