FACEBOOK NDIO CHANZO CHA KIFO CHAKE

Mitandao ya kijamii imekuwa sehemu ya furaha na burudani, ingawa pia ni chanzo kikubwa cha habari za aina zote.  Lakini inaweza kuwa chanzo cha matatizo makubwa
kwa wanaoitumia pia
.

Ripoti kutoka Buffalo, New York, Marekani zinaeleza kuwa kijana mwenye umri wa miaka 15 anaefahamika kwa jina la James Shores amepoteza maisha baada ya kushiriki katika challenge ya facebook ya kujiunguza na moto mwili mzima huku unajirekodi kisha unapost kipande cha video ili watu waone kwa sekunde chache utakavyofanya. 

Tahadhari ni kwamba baada ya maumivu ya sekunde chache unajipiga maji ili kujiokoa.
Challenge hiyo maarufu imepewa hashtag  #FireChallenge katika mtandao wa kijamii wa Facebook.
Lakini kama wahenga wanavyosema usicheze na moto, James Shores alipoteza maisha baada ya kufanya zoezi hilo na kuzidiwa na moto uliomchoma mwili mzima huku jitihada za kujiokoa zikishindikana.

Vyanzo vimeeleza kuwa hata marafiki zake waliokuwa wanamchukua kipande cha video walijaribu kupambana na moto huo lakini walishindwa kabisa kumuokoa kwa muda kwani baada ya moto huo kuzima alipoteza maisha kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata.
Inaelezwa kuwa wengi ambao wamekuwa wakishiriki katika shindano hilo hujiwasha moto wakiwa karibu na bafu kwa sekunde chache na kisha kujirusha ndani ya maji.

Kamishina wa Polisi wa Buffalo, James Daniel aliongea na News-Two na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiwaonya watu kuacha kushare video za namna hiyo kwani zinaweza kuwa tatizo kubwa hasa kwa watoto.
Facebook pia wameamua kuzifuta video za aina hiyo #FireChallenge kutoka kwenye website yao.

Popular Posts