HUYU NDIO MKENYA ALIESAJILIWA NA CLUB YA LIVERPOOL
Baada ya juzi usiku kukamilisha usajili wa Dejan Lovren, klabu ya Liverpool imeendelea kujiimarisha katika kikosi chao kwa kufanya usajili mwingine leo hii.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Belgium Divock Origi ndio mchezaji mpya aliyejiunga na kikosi cha Brendan Rogers akitokea Lille ya Ufaransa kwa ada ya uhamisho wa £10m.
Origi, mwenye miaka 19 amesaini mkataba wa miaka mitano lakini atabakia Lille kwa mkopo wa mwaka mmoja na atahamia Anfield msimu ujao.
Origi alianza maisha yake ya soka katika klabu ya Genk kabla ya kuhamisa Lille akiwa na miaka 15.
Mchezaji huyu wazazi wake ni wakenya, lakini alichagua kuichezea Belgium na aliiwakilisha nchi kwenye michuano ya kombe la dunia iliyoisha hivi karibuni.