TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE
Kiungo wa Manchester United Marouane Fellaini huenda akaondoka kwenda Napoli baada ya kufanya mazungumzo na mkuu wa klabu hiyo Riccardo Bigon (Daily Express),United pia huenda wakamruhusu Shinji Kagawa, 25 kuondoka huku Borussia Dortmund
wakiwa tayari kumchukua tena (Independent), Chelsea watalazimika kumuuza kipa Petr Cech, 32, kwenda PSG iwapo watashindwa kumuuza Fernando Torres, 30, au John Obi Mikel, 27 (Daily Telegraph), meneja wa Southampton Ronald Koeman ana matumaini ya kumsajili kiungo Serge Gnabri, 19 na Carl Jenkinson, 22 kutoka Arsenal (Daily Star), hata hivyo Southampton wanakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa West Ham wanaokaribia kumchukua Jenkinson kwa mkopo (Daily Mirror),
beki wa kulia wa Sporting
Lisbon Miguel Lopez, 27 anajiandaa kujiunga na Tottenham kwa mkopo, huku
akitazamia uhamisho wa kudumu baadaye (Daily Mail), meneja wa Liverpool
Brendan Rodgers amethibitisha kuwa hawatopanda dau tena kumchukua Loic
Remy (Daily Mirror), lakini Newcastle United huenda wakajaribu kumchukua
tena Remy kwa mkopo (Goal.com) meneja wa Aston Villa
Paul Lambert
anataka kumsajili Victor Moses, 23, kwa mkopo na pia kumchukua Ki
Sung-yeung, 25 kutoka Swansea wiki hii (Daily Telegraph), wakala wa
Samuel Eto'o amewaambia West Ham kuwa mchezaji huyo yuko huru kujiunga
nao, kuziba pengo la Andy Carroll aliyeumua, lakini Eto'o
anataka
mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki (Daily Mail), mkurugenzi mkuu wa
Juventus Beppe Marotta amesema klabu yake itajitahidi kutomwachilia
Arturo Vidal, na kutupilia mbali taarifa kuwa mchezaji huyo anakwenda
Chelsea (Tottosport), Southampton wanafikiria kumchukua beki wa kati wa
Sporting Lisbon Marcos Rojo, 24, kufutia kuondoka kwa wachezaji wengi
Saints (Le Figaro), Atletico Mineiro amethibitisha kuondoka kwa kiungo
wa zamani wa Barcelona Ronaldinho, 34
(L'Equipe), mshambuliaji wa
Ubelgiji Divock Origi, 19, amesaini mkataba wa miaka mitano na Liverpool
(Bild), PSG wameruhusu mshambuliaji wao Ezequiel Lavezzi, 29, kwenda
Atletico Madrid. Mchezaji huyo anasakwa pia na Liverpool (AS.com) Lazio
ya Italia imetangaza kuwa inamchukua beki wa Feyenoord Stefan de Vrij,
22 (L'Equipe). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!
(4 photos)