TETESI ZA SOKA ULAYA


Liverpool wamemuulizia mshambuliaji wa Southampton Jay Rodriguez, 24, baada ya uhamisho wa Loic Remy wa pauni milioni 8.5 kuporomoka (Talksport), Manchester United wameambiwa watatakiwa kulipa pauni milioni 79 kama wanamkata kiungo wa Roma Kevin Strootmam, 24, licha ya mdachi huyo kuwa majeruhi tangu mwezi Machi (Sun), beki wa Ubelgiji Jan Vertonghen, 27, amesema atasaini mkataba mpya na Tottenham, licha ya Barcelona kumnyatia (Daily Mirror), winga wa Real Madrid Angel Di Maria, anataka kujiunga na Manchester United baada ya kughadhibishwa na PSG kumtaka kwa mkopo na hataki kurejea Bernabeu (Daily Star), hata hivyo kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti amesena anamtarajia kurejea kambini tarehe 5 Agosti (AS), wakati huohuo gazeti la Marca linasema uhamisho wa Di Maria kwenda PSG utatangazwa wiki ijayo katika mkataba wa pauni milioni 51. Juventus watajaribu kutoa dau kumtaka mshambuliaji wa Chelsea Romelu Lukaku, 21, kuimarisha kikosi chao ingawa wanakabiliana na ushindani mkali kutoka Real Madrid (AS.com) Barcelona wameanza tena kumuulizia beki wa Liverpool Daniel Agger, 29 (Le Figaro), Arsenal wamempa mkataba wa miaka mitano kipa wa Real Madrid Iker Casillas, 33 (Bild) meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola anataka kumchukua kipa wa zamani wa Barcelona Victor Valdes, 32 (AS.com), Barcelona wametangaza kumsajili winga kutoka Brazil, Ferrao, 24 kutoka Tyumen ya Urusi (Mundo Deportivo). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Kwa walioswali Eid leo- Eid Mubarak, kwa wanoendelea kufunga, Saum Maqbul. Cheers!
Salim Kikeke's photo.
Salim Kikeke's photo.
Salim Kikeke's photo.

Popular Posts