Alonso afuata nyayo za Xavi Hernandez wa FC Barcelona

Kiungo wa klabu bingwa barani Ulaya, Real Madrid, Xabi Alonso ametangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Hispania baada ya kuitumikia timu hiyo katika michezo 114.

Alonso mwenye umri wa miaka 32 ametangaza maamuzi hayo baada ya kiungo mwenzake Xavi wa FC Barcelona kutangulia kustaafu kuitumikia timu ya taifa siku chache zilizopta.
Alonso ametangaza maamuzi ya kustaafu soka kwa upande wa timu ya taifa, kupitia mtandao wa kijamii wa tweeter ambapo anaamini kwenye mtandaio huo habari hizo zitawafikia mashabiki wake kwa haraka zaidi.
Ujumbe wake katika mtandao huo wa kijamii unaeleza kwamba "Nimeamua kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Hispania, baada ya miaka 11 kuitumikia timu hiyo.”
Kiungo huyo alikuwa sehemu ya kikosi cha Hispania kilichokubali kufungwa mabao matano kwa moja dhidi ya Uholanzi katika mchezo wa kwanza wa kundi la pili kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 zilizochezwa nchini Brazil.
Pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Hispania kilichotwaa ubingwa wa barani Ulaya mara mbili mwaka 2008 na 2012 pamoja na ubingwa wa kombe la dunia mwaka 2010 baada ya kuifunga Uholanzi bao moja kwa sifuri.

Popular Posts