CiCi Bellis aweka rekodi ya dunia US Open

Mwanadada mwenye umri wa miaka 15, CiCi Bellis, ameustaajabisha ulimwengu wa Tennes baada ya kumtupa nje ya michuano ya US Open inayoendelea jijini New York nchini Marekani gwiji wa mchezo huo Dominika Cibulkova.

Bellis, ambaye anashika nafasi ya 1,208 kwa ubora duniani upande wa wanawake amefanikisha azma hiyo kwa kumshinda Cibulkova ambaye anashika nafasi ya 12 kwa ubora duniani kwa seti mbili kwa moja ambazo ni 6-1, 4-6 pamoja na 6-4.
Mafanikio hayo yanamfanya Bellis, kuweka rekodi ya kuwa mshiriki mwenye umri mdogo wa kike kupata ushindi na kusonga mbele kwenye michuano ya US Open, tangu mwanadada  Anna Kournikova, kutoka nchini Urusi  kushinda mchezo wake na kutinga kwenye mzunguuko wa nne mwaka 1996 ambapo alikuwa na umri wa miaka 15 na siku 152.
Bellis kwa sasa ana umri wa miaka 15 na siku 59 hivyo anaweka rekodi nyingine katika michuano yote mikubwa ya mchezo wa Tennis duniani (Grand Slam).

Popular Posts