GARI LATEKETEA KWA MOTO MOROGORO
Gari dogo likiteketea kwa moto leo maeneo ya Msamvu mkoani Morogoro.
Gari la zimamoto likiwa limefika na kuanza kazi ya kuuizima moto huo.
Zoezi la uzimaji wa moto huo likiendelea.
Wananchi wakishuhudia janga la moto lililotokea.
GARI dogo ambalo halikupatikana namba zake limeteketea kwa moto leo
maeneo ya Msamvu mkoani Morogoro. Mpaka mpigapicha hizi akiondoka eneo
la tukio, chanzo cha moto huo kilikuwa bado hakijafahamika.chanzo GLOBAL PUBLISHERS