Hodgson:England haijapoteza uelekeo
Kocha wa timu ya Taifa ya
England Roy Hodgson amesema England haijapoteza uelekeo wakati
ikijiandaa na michuano ya kombe la ulaya mwaka 2016, na kuelekea kampeni
za kufuzu kushiriki michuano hiyo, kampeni zitakazoanza mwezi ujao.
England ambayo ilishindwa kufanya vizuri kwenye michuano ya kombe la dunia katika hatua ya makundi itaanzia kampeni yake ugenini kwa kupambana na Switzerland tarehe 8 mwezi Septemba.
Katika katika kundi iliyopangwa, England itapambana na timu za Slovenia,Estonia, Lithuania na San Marino.
Hodgson amesema ana matumaini kuwa watafanya vizuri.
England imeshuka kiwango cha ubora vya fifa mpaka nafasi ya 20th baada ya kuchemka nchini Brazil walipopoteza mchezo dhidi ya Italia na Uruguay, kabla ya kupata pointi dhidi ya Costarica ambapo tayari walikuwa wametolewa.