LAMPARD ASTAAFU SOKA LA KIMATAIFA
Frank Lampard ametangaza kustaafu kucheza soka la kimataifa. Kiungo
huyo, aliyejiunga na Manchester City kwa mkopo akitokea New York City,
alicheza mechi yake ya mwisho kama nahodha wa England katika sare ya
0-0 dhidi ya Costa Rica katika michuano ya Kombe la Dunia, mwezi Juni.
Kiungo huyo wa zamani wa Chelsea, 36, ameichezea timu yake ya taifa mara
106, tangu Oktoba mwaka 1999, alipocheza mechi yake ya kwanza dhidi ya
Ubelgiji. Lampard amecheza katika michuano mitano mikubwa na kupachika
mabao 29. Anakuwa mchezaji wa sita kuwahi kuichezea England mara nyingi
zaidi sawa na Sir Bobby Charlton. Lampard, aliyeanza kucheza soka la
kulipwa katika klabu ya West Ham, aliondoka Chelsea msimu uliopita baada
ya kuichezea klabu hiyo mara 648 na kufunga magoli 211.
