Man Utd yatangaza vita na Arsenal zikisalia siku nne ...
Katika kuhitaji kujiimarisha kabla ya dirisha la usajili
halijafungwa usiku wa manane siku ya jumapili, Man Utd wamejikuta
wakiingia vitani na wapinzani wao Arsenal kwenye mipango ya kumuwania
kiungo mkabaji kutoka nchini Ureno na klabu ya Sporting Lisbon William
Carvalho.
Man Utd wameingia katika vita hiyo ikiwa ni awamu yao ya pili kuonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22, lakini kati kati ya mwezi uliopita walijiondoa na kuipisha Arsenal ambayo ilitajwa kuwa na mipango ya kumpeleka nchini Uingereza.
Man Utd wameonyesha lengo hilo kwa mara ya pili huku uongozi wa klabu ya Sporting Lisbon ukiwa umeshawaarifu Arsenal kutoa kiasi cha paund million 24, ili waweze kukamilisha dili hilo.
Hata hivyo bado haijafahamika kama klabu hizo za nchini Uingereza zimeshatuma ofa mjini Lisbon kwa ajili ya kuanza vita ya kumuwania William Carvalho ama la.
Carvalho alionyesha kiwango kizuri wakati wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 ambazo zilifanyika nchini Brazil, japokuwa timu yake ya taifa ya Ureno iliondolewa mapema katika hatua ya makundi.