Miley Cyrus amtetea kijana wake wa Mtaani anaesakwa na polisi

Baada ya kuripotiwa habari kuwa kijana wa mtaani, Jesse Helt aliyepanda jukwaani na Miley Cyrus wakati wa utoaji tuzo za MTV VMAs anasakwa na polisi kwa kosa la kuvunja masharti ya probation, Miley Cyrus amemtetea kupitia akaunti yake ya Twitter.

Miley amevilaumu vyombo vya habari kwa kujikita katika habari ya yeye kusakwa na polisi badala ya kuripoti zaidi kuhusu tatizo la vijana  wasio na makazi alilolizungumzia katika jukwaa hilo.
Jesse Helt alipanda jukwaani na Miley Cyrus na kupokea tuzo ya video bora ya mwaka kwa niaba yake na kisha kutoa hotuba fupi kuhamasisha watu kuliangalia tatizo la vijana wanaoishi katika mazingira magumu (wasio na makazi).
Siku moja baada ya tukio hilo, iliripotiwa kuwa kijana huyo anatafutwa muda mrefu na polsi wa Oregon.

Popular Posts