Louis van Gaal: Di Maria ni mchezaji mwenye ubora
Mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Argentina Ángel Fabián
Di María Hernández, amekamilisha ndoto za kucheza ligi ya nchini
Uingereza, baada ya kusaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Man Utd
Di Maria, amejiunga na mashetani wekundu akitokea nchini Hispania alipokuwa akiitumikia klabu bingwa barani Ulaya, Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa paund million 59.7.
Usajili wa winga huyo mwenye umri wa miaka 26 unaweka rekodi mpya ya gharama kubwa ya usajili katika soka la nchini Uingereza kwa kuiondoa rekodi ilikuwa imewekwa na mshambuliaji kutoka nchini Hispania Fernando José Torres Sanz ambaye alisajiliwa na klabu ya Chelsea kwa ada ya uhamisho wa paund million 50 akitokea kwenye klabu ya Liverpool mwaka 2011.
Kusajiliwa kwa Di Maria kumempa nafasi ya meneja wa klabu ya Man Utd Louis van Gaal kuzungumza chochote mbele ya vyombo vya habari ambapo amesema mchezaji huyo ana ubora wa viwango vya kimataifa na anaamini kwenda kwake Old Trafford huenda kukaleta mabadiliko.