Ndoa ya Angelina na Brad Pitt: Brad Pitt aonesha pete ya ndoa, fahamu wageni waliohudhuria (Picha)

Brad Pitt na Angelina Jolie walifunga ndoa Jumamosi iliyopita nchini Ufaransa na taarifa za ndoa yao zilitolewa wiki hii na msemaji wao.

Kwa mujibu wa E!News , tukio hilo lilihudhuriwa na watu 22 tu na inaelezwa kuwa Angelina Jolie alivaa gauni jeupe ya kitamaduni iliyomfanya aonekane mwenye mvuto zaidi katika siku hiyo maalum kwao.
Chanzo kimeiambia MailyOnline kuwa Angie na Brad waliamua kufunga ndoa katika jumba walilolinunua mwaka 2011 baada ya Angelina kumuahidi mama  yake kuwa atafunga ndoa nchini Ufaransa.
 Chanzo hicho kimeongeza kuwa ndoa hiyo ni sehemu ya kumbukumbu ya miaka 10 tangu walipokutana wakati wa kushuti filamu ya Mr. and Mrs. Smith na kuanzisha uhusiano wao.
Brad Pitt ameonesha pete ya ndoa:

Eneo linaloaminika kuwa wawili hao walifungia ndoa

Popular Posts