Ofisi ya usalama yashambuliwa Mogadishu
Shambulio dhidi ya makao makuu ya idara ya usalama ya Somalia mjini Mogadishu limeuwa watu 10.
Wakuu walisema saba kati ya hao ni wapiganaji wa al-Shabaab ambao waliingiza kwa nguvu gari lilojaa mabomu katika uwa wa jengo hilo ambalo lina ulinzi mkali.
Tena washambuliaji walijaribu kuingia ndani ya jengo.
Al-Shabaab ilisema ilifanikiwa kuwaachilia huru wafungwa wengi katika makao makuu hayo, ambayo yana gereza chini kwenye handaki na pahala pa kuhoji wafungwa.