TETESI ZA SOKA ULAYA
Boss wa Manchester United Louis van Gaal anataka kumsajili kiungo wa
Juventus Arturo Vidal, 27, kwa mkataba wa pauni milioni 34 kiasi ambacho
kitafikisha pauni milioni 200 za kununua wachezaji Old Trafford katika
kipindi cha miaka miwili (Independent),
United huenda wakamtoa Javier Hernandez, 26, kwenda Juventus, katika
mkataba wa Vidal (Daily Express), Manchester United pia wanatarajia
kutaka kumsajili Daley Blind, 24 kutoka Ajax kwa pauni milioni 18 katika
siku chache zijazo (Sun), Arsenal wanaonekana kuzidiwa kete na Roma,
kumsajili beki wa kati Kostas Manolas,
23 kutoka Olympiakos (Goal),
Manchester United na Arsenal wamepata matumaini ya kuendelea kumfuatilia
beki wa Roma Mehdi Benatia, 27, baada ya klabu hiyo ya Italia kuvunja
mazungumzo na Bayern Munich (Daily Star), Arsenal huenda wakamfuatilia
Danny Welbeck, 23, kutoka Man United, au Loic Remy, 27, kutoka QPR
kuziba pengo la Olivier Giroud ambaye huenda akakosa kucheza kwa miezi
mitatu kutokana na jeraha la kiwiko cha mguu
(Daily Telegraph),
Southampton wameanza kumfuatilia beki wa Atletico Madrid Toby
Alderweireld, 25, na kuwazidi Monaco (Times), Tottenham wapo tayari
kutoa pauni milioni 8 kumchukua nahodha wa Sevilla Federico Fazio, 27
(London Evening Standard) Chelsea wanazungumza na Roma kumchukua Mattia
Destro, 23 (Daily Mirror), QPR wanakaribia kumsajili beki wa Liverpool
Jack Robinson, 20 kwa mkataba wa pauni milioni 1 (Daily Mirror), West
Ham wamemuulizia beki wa kati wa Bayer Leverkusen Philipp Wollscheid,
25, (Daily Mail),
Sunderland, QPR na West Brom wanamtaka kiungo wa
Leicester Andy King, 25, (Sun), AC Milan bado wanataka kumchukua
Fernando Torres kutoka Chelsea, wakala wake akipendekeza kumchukua kwa
mkopo, ingawa mshahara wake mkubwa unaonekana kuwa kikwazo (Metro),
Napoli wataanza kumfuatilia tena kiungo wa Tottenham, Sandro kwa mkopo
(The Times), Sporting wamewaambia Arsenal kuwa watakubali kitita cha
euro milioni 30 kumsajili William Carvalho, kama Arsenal watakubali
kumtoa Serge Gnabry, Francis Coquelin au Yaya
Sanogo kwa mkopo (The
Times), Everton wanakaribia kukamilisha usajili wa Samuel Eto'o. Roberto
Martinez alikuwa akimtaka Danny Welbeck wa Man United, lakini
alikatishwa tamaa na bei ya Pauni milioni 15 (The Times) na boss wa
Inter Milan, Walter Mazzarri amewaambia watu wake kuwa wako huru
kujaribu kumsajili Ezequiel Lavezzi kutoka Paris St-Germain
(Tuttosport). Zimesalia siku sita kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Share hizi na wapenda soka wote.
Cheers!!