Uhodari wa Jotevic dhidi ya Liverpool wamtia pilipili Pallegrini
Meneja wa klabu bingwa nchini Uingereza Man City, Manuel
Pellegrini amempongeza mshambuliaji kutoka nchini Montenegro Stevan
Jovetic, kufuatia juhudi alizozionyesha usiku wa kuamkia hii leo wakati
wa mchezo dhidi ya
Liverpool.
Pellegrini, amesema Jotevic alionyesha uwezo mkubwa sana wakati wa mchezo huo na hatua ya kufunga mabao mawili kati ya mabao matatu yaliyoipa ushindi Man City, ameichukuliwa kama changamoto mpya katika safu yake ya ushambuliaji.
Amesema mshambuliaji huyo mara kadhaa alikuwa anakabiliwa na changamoto ya kuwania nafasi katika kikosi cha kwanza, lakini uhodari na umakini aliouona jana, hana budi kutumia fursa ya kumpa nafasi kila mara ili aweze kuongeza ushindani wa kuwania namba dhidi ya washambuliaji wengine.
“Alicheza vizuri sana na alikuwa kama chagizo la ushindi mzuri tulioupta hii leo, sina budi kuhakikisha namtumia mara kwa mara ili kuona uwezekano wa kuongeza kasi ya kuwania nafasi ya ushambuliaji miongoni mwa wachezaji wanaocheza nafasi hiyo.” Amesema mzee huyo kutoka nchini Chile
Katika mchezo huo Liverpool waliokuwa wanashuhudiwa na mshambuliaji wao mpya Mario Balotelli walishindwa kufua dafu mbele ya Man City kutokana na kiwango duni walichokionyesha.
Bao lingine la Man City katika mchezo huo lilifungwa na mshambuliaji kutoka nchini Argentina Sergio Agüero aliyeingia kuchukuwa nafasi ya Edin Dzeko katika dakika ya 69.