Utafiti: Marijuana imesaidia kupunguza vifo katika nchi zilizoiruhusu

Kuna msemo unaoeleza kuwa kila kitu kina faida na hasara, hasara inapokuwa kubwa kuliko faida basi hicho kitu kinakuwa sumu na hakikubaliki, ndivyo ilivyo Marijuana kwa Tanzania na imewekwa kati ya dawa za kulevya zisizoruhusiwa kisheria kwa manufaa ya Taifa.

Lakini kwa mujibu wa CNN, utafiti uliofanywa na wanasayansi na kuchapishwa kwenye JAMA Internal Medicine Journal umebaini kuwa nchi/states ambazo zimeruhusu uvutaji wa marijuana kama sehemu ya matibabu zimepunguza sana idadi ya vifo vinavyotokana na utumiaji kupita kiasi wa dawa za kutuliza maumivu (painkiller overdoses).
Kwa mujibu wa utafiti huo, maeneo yaliyopitisha matumizi ya marijuana kama dawa yamepata upungufu wa vifo 1,700 vilivyokuwa vikiripotiwa tangu mwaka 2010.
“Tumekuta kulikuwa na upungufu wa vifo kwa 25% vilivyokuwa vinatokana  vya matumizi ya dawa za kupunguza maumivu kupita kiasi (overdose).” Dr. Marcus Bachhuber ameiambia CNN.
Hata hivyo, tatizo la watu kupoteza maisha kutokana na kutumia dawa za kutuliza maumivu kupita kiasi kwa Tanzania halina uhusiano na matumizi ya marijuana kwani idadi ya watu wanaopoteza maisha kwa kutumia dawa za kutuliza maumivu hufanya hivyo kutokana na kukosa elimu au kutofuata maelekezo ya daktari kwa kutaka wanywe nyingi ili wapone haraka.
 Lakini wengine (idadi ndogo) hutumia dawa hizo kwa lengo la kutaka kujiua. Madhara hasi ya marijuana ni makubwa zaidi kwa jamii ya watanzania.

Popular Posts