Afisa Wa FIFA: Qatar Hawatokuwa Wenyeji Wa Fainali Za Kombe La Dunia 2022
Afisa wa ngazi za juu za shirikisho la soka duniani FIFA,
ametoboa siri na kueleza hadharani mpango wa nchi ya Qatar kuwa mbioni
kupokonywa nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka
2022.
Theo Zwanziger ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya FIFA amesema kuna uwezekano mdogo kwa nchi hiyo kuendelea kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2022, kutokana na mapandekezo yanayoendelea kutolewa kufuatia taratibu mbali mbali za kiafya zinazofanywa.
"Kwangu binafsi sianimi kama mwishoni mwa mwaka 2022, fainali za kombe la dunia zinaweza kufanyika nchini Qatar, kutokana na hali ya hewa ya nchi hiyo," Afisa huyo kutoka nchini Ujerumani ameiambia Sport Bild hii leo.
"Wataalamu wa masuala ya kiafya wameshapingana na pandekezo la fainali, hizo kufanyika mwishoni mwa mwaka ambapo katika ukanda wa mashariki ya kati nchi nyingi zinadai huwa zinapata majira ya maridi," Ameongeza mtendaji huyo wa zamani wa shirikisho la soka nchini Ujerumani (DFB).
Pamoja na madai hayo ya kiongozi huyo ambayo yanachukuliwa kama hatua ya kuvujisha siri ya kinachoendelea ndani ya FIFA, kufuatia sakata nchi ya Qatar kupokonywa uenyeji wa fainali za kombe la dunia, tayari siku za nyuma ilielezwa kwamba licha ya mwishoni mwa mwaka kuwa na majira ya baridi, pia kamati ya maandalizi ya fainali hizo kwa mwaka 2012 ilipendekeza kufunga mitambo ya kupunguza hali ya joto viwanjani.
"Wanachotakiwa kufanya ni kufunga vifaa vya kupunguza joto viwanjani, kitendo ambacho sidhani kama FIFA wanaweza kukubaliana nacho,"
"Mashabiki wa soka watasafiri kutoka kila pande za dunia na itakuwa ni mara yao ya kwanza kukutana na hali ya joto kali, hivyo huenda ikatokea madhara makubwa na pengine kusababisha vifo". Ameongeza Zwanziger.
Sababu nyingine iliyotajwa na mjumbe huyo wa kamati ya utendaji ya FIFA ni hatua ya kupingwa kwa utaratibu wa kuahirishwa kwa ligi nyingi barani Ulaya na kwingineko ambazo huanza mwezi August na kumalizika mwezi May, hivyo kama fainali hizo zitapitishwa na kuchezwa mwishoni mwa mwaka italazimika ratiba za ligi hizo kuvurugwa.
Wakati sakata hilo likiibuka, FIFA pamoja na kamati ya maandalizi ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2022 bado wanaendelea kujadili na kumsaka mchawi kufuatia madai ya kutolewa kwa Malungula wakati wa mchakato wa kuichagua Qatar mwaka 2010 kabla ya kutangazwa kuwa mwenyeji wa fainali hizo.