Alichokifanya Chris Brown baada ya msichana asiyemjua kutaka kumkiss akiwa na Karrueche

Chris Brown ameingia tena matatizoni baada ya kumzingua shabiki wa kike anaedaiwa kumrukia na kujaribu kumkiss mbele ya mrembo wake Karrueche Tran katika Club moja ya usiku.

Kwa mujibu wa TMZ, mwimbaji huyo wa ‘Loyal’ aliyekuwa na onesho katika club hiyo huko Texas, badala ya kuwaacha walinzi wake wamshughulikie msichana huyo kwa hasira alimsukuma vibaya.
Vyanzo vimeieleza Hollywoodlife kuwa mama mzazi wa Chris Brown na mpenzi wake wamekuwa na hofu kubwa kufuatia matatizo mfululizo yanayomtokea mwimbaji huyo.
Chris Brown alishauriwa hivi karibuni kutojiingiza katika matatizo baada ya kutoka jela hivi karibuni alikotumikia kifungo cha siku 108 kwa kosa la kuvunja masharti ya kipindi cha matazamio.

Popular Posts