Amber Rose avunja ukimya tuhuma za kuchepuka na mme wa Mariah Carey, aeleza chanzo cha kumuacha Wiz Khalifa
Baada ya taarifa hizo kusambaa kwenye vyombo vya habari siku mbili zilizopita, iliripotiwa kuwa chanzo cha yote ni Amber Rose kuchepuka na mme wa Mariah Carey, Nick Cannon ambaye pia ndoa yake iko katika sintofahamu.
Hata hivyo, Amber Rose amethibitisha kuwa Wiz Khalifa alikuwa akimsaliti na wanawake wengine huku akikanusha vikali tuhuma za kuchepuka na mwanaume yeyote kwa kipindi chote cha ndoa yao.
Ameendelea kusisitiza kuwa hivi sasa anakijikita katika malezi ya mtoto wao wa kiume, Sebastian.
Amber ameandika tweet kadhaa kupitia twitter kuhusu sakata hilo.
“Please stop with the fake stories. I would never ever ever cheat on my husband in a million years I think u guys know this..... Unfortunately my now ex husband can't say the same…. I'm devastated and crushed but my main focus is Sebastian. Thank u for all the support in this difficult time.”