Arsene Wenger: Naiheshimu Sana Southampton

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema klabu ya Southampton huenda ingekuwa bora zaidi msimu huu endapo ingeendelea kuwa na wachezaji mahiri ambao kwa asilimia kubwa walikuzwa na kituo cha kulea vijana cha klabu hiyo.

Wenger ameizungumzia klabu hiyo yenye maskani yake kwenye uwanja wa mtakatifu Maria, kufuatia mshike mshike ambao hii leo utakwenda kuwakabili The Gunners katika michuano ya Capital One Cup dhidi ya The Saints.
Amesema Southampton ni klabu bora nchini Uingereza na miaka yote imekuwa ikitoa wachezaji wazuri kutokana na mikakati waliyojiwekea hivyo anaamini mambo yangekuwa mazuri zaidi endapo wangeendelea kuwa na wachezaji waliokubali kuwauza kwenye klabu nyingine.
Hata hivuo mzee huyo kutoka nchini Ufaransa amesema pamoja na kuonyesha masikitiko hayo dhidi ya The Saints bado klabu hiyo inaonekana kuwa makini katika kusaka mafanikio na ndio maana mpaka sasa ipo kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya nchini Uingereza kwa tofauti ya point tatu dhidi ya vinara wa ligi hiyo Chelsea.
Mwanzoni mwa msimu huu Southampton walikubalia kuwauza wachezaji saba wenye viwango vya hali ya juu katika klabu za nchini UIngereza ambao ni Adam Lallana, Rickie Lambaert, Colum Chambers, Dejan Rovren, Luke Shaw, Billy Sharp pamoja na Jonatham Forte.
Wachezaji wengine waliokuzwa na kuondoka kwenye klabu hiyo ni Gareth Bale, Alex Oxlade-Chamberlain pamoja na Theo Walcott.
Arsenal hii leo itapambana na Southampton katika uwanja wa Emirates.

Popular Posts