Asilimia 70 ya wanajeshi wa Marekani wapinga upelekaji vikosi vya ardhini Iraq na Syria

Wakati Majeshi ya anga ya Marekani yakiendelea na mashabulizi nchini Iraq na Syria kulenga kundi linalojiita Islamic States of Iraq and Syris (ISIS), idadi kubwa ya wanajeshi wa Marekani wamepinga
hatua inayotaka kuchukuliwa na rais Barack Obama kupeleka vikosi vya ardhini katika nchi hizo.
Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na Military Times, 70% ya wanajeshi wa vikosi vya ardhini waliohojiwa wamepinga upelekwaji wa vikosi hivyo Iraq na Syria huku 25% tu ikiunga mkono.
Matokeo hayo yanatokana na uamuzi wa awali wa kupeleka vikosi vya ardhini vya Marekani nchini Iraq katika harakati za kuung’oa utawala wa Saddam Hussein ambapo wanajeshi wengi wa Marekani walipoteza maisha.
Chanzo: UStoday

Popular Posts