Ay kushuti video ya 'It's Going Down' Marekani, asema ni kuepusha gharama

Mzee wa Commercial, AY amepanga kufanya video kubwa ya wimbo wake ‘It’ Going Down’ aliowashirikisha Ms Trinity na Lamyia, na eneo la tukio litakuwa Miami, Marekani.

AY ameeleza kuwa ameamua kufanya video hiyo nchini Marekani ili kuepuka gharama za kuwasafirisha wasanii aliowashirikisha kwenye wimbo huo kuja nchini Tanzania.
“Ni kuepusha baadhi ya gharama kwa sababu ukisema Trinity aje huku, Trinity hasafirigi peke yake, Lumiaya hasafiri peke yake. Hapo unaweza kushangaa unalipa tiketi zako sita au saba.” Amesema.
AY amesema amepanga kuanza kushuti mapema October na kwamba video itatoka mwezi huo huo.
Audio ya wimbo huo imetayarishwa katika moja ya studio kubwa California, Marekani.

Popular Posts