Brendan Rodgers: Mario Balotelli Sio Msumbufu

Baada ya kupoteza mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya West Ham, majogoo wa jiji Liverpool hii leo watajiuliza tena mbele ya Middlesbrough katika mchezo wa kuwania kombe la ligi *Capital One Cup* huko nchini.

Kuelekea katika mchezo huo ambao utachezwa katika uwanja wa Anfield meneja wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers amesema hana shaka na kikosi chake kutokana na uhalisia wa mambo yalivyoonekana katika majuma mawili yaliyopita ambapo walipoteza michezo miwiwli mfululizo.
Rodgers amesema kikosi chake kipo imara na kitakuwa tayari kufanya linalowezekana ili kufanikisha njia ya kurejea katika mstari wa ushindi kama ilivyokuwa mwanzoni mwa msimu huu.
Katika hatua nyingine meneja huyo kutoka Ireland ya kaskazini amesema anafurahia kufanya kazi na mshambuliaji kutoka nchini Italia Super Mario Barwuah Balotelli na wala hajaona mapungufu yake kama ilivyokuwa inafikiriwa hapo awali.
Amesema tangu alipomsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, maisha yamekuwa safi na amekuwa anashirikiana na wachezaji wengine klabuni hapo kwa kuzingatia taratibu na sheria zilizowekwa.

Popular Posts