Cheikhou kukosa mechi tano za ligi kuu

Kiungo wa kati, wa West Ham Cheikhou Kouyate hatashiriki michuano ya ligi kuu ya England kwa wiki sita kutokana na jeraha alilolipata kwenye korodani.

Kouyate aliumia wakati wa mechi ya siku ya jumamosi ambapo West Ham iliinyuka Liverpool mabao matatu kwa moja.
Kiungo huyo huenda akakosa michezo mitano ya ligi kuu ya England iliyo mbele yao ukiwemo ule wa dhidi ya Manchester United utakaopigwa tarehe 27 mwezi huu.

Popular Posts