CUF yalaani vikali Jeshi la Polisi kuwashambulia waandishi wa habari

Chama cha Wananchi-CUF, kimelaani vikali kitendo cha Jeshi la polisi kuwashambulia waandishi wa habari wakati wapo kazini kwa lengo la kutafuta habari

Mashambulizi hayo yalitokea wakati waandishi hao wakiwa wanasubiri hatma ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA, Freeman Mbowe akiwa katika mahojiano kwenye Makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam Alhamis iliyopita
Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CUF  Profesa Ibrahim Lipumba amesema kwamba ipo haja kwa sheria kufuatwa kwani waandishi wana uhuru wa kupata habari na si kunyimwa.
Aidha, Profesa Lipumba amesema  hatua kali zichukuliwe kwa kiongozi aliyetoa ruhusa kwa askari hao kuwapiga waandishi.

Popular Posts