Hazard Awamaliza Viongozi Wa PSG Wanaohaha Kwa Miaka Miwili Kumsaka
mapenzi yake ya dhati kwa The Blues.
Hazard, mwenye umri wa miaka 23 amefanya hivyo baada ya kuchoshwa na minong’ono inayoendelea nchini Ufaransa ambayo inadai yu njini kujiunga na klabu bingwa nchini humo.
Akihojiwa na kituo cha televisheni cha nchini Ufaransa cha Canal+, Hazard amesema tangu mwaka 2012 amekuwa akihusishwa na minong’onio hiyo lakini ukweli ni kwamba anahisi alipo sasa panamfaa zaidi.
Kauli ya kiungo huyo aliyesajiliwa na The Blues akitokea Lille ya nchini Ufaransa inakwenda sambamba na ile iliyotolewa na meneja wa klabu ya Chelsea mwishoni mwa juma Jose Mourinho ambapo alinukuliwa na vyombo vya habari akisema Hazard hana pakwenda zaidi ya kuendeleza furaha yake hapa.
Hazard amesema, “Nipo safi na ninajihisi ni mwenye furaha wakati wote ninapocheza hapa (Chalsea) na sioni sababu ya kuanza kufikiria kurudi katika ligi ya nchini Ufaransa Ligue 1.”
“Hata kama itatokea naondoka hapa na kulazimika kurejea katika ligi ya nchini Ufaransa, nitahakikisha ninacheza katika klabu yangu niliyoizoea ya Lille”.
“Ligi ya nchini Ufaransa (Ligue 1) ni ligi kubwa katika ukanda wa bara la Ulaya na mara nyingi imekuwa ikiwahusha sana wachezaji wenye umri mdogo na kwa hilo sina budi kujisifia kwa sababu nami nilikuwa mmoja wao.”
“Kila mwaka nimekuwa nahusishwa na harakati za kutaka kusajiliwa na PSG na hatua hiyo imeshindikana mara zote, sasa kwa nini inaendelea kuzungumzwa ili hali imeshafahamika haiwezekani?” Amehoji Hazard
“PSG hawana tofauti na klabu ninayoitumikia sasa (Chelsea) na sioni sababu ya kufikiria kurejea huko na kuwatumikia, zaidi ya kuendelea kucheza kwa kujihakikishia nafasi hapa nilipo.” Ameongeza Hazard
Eden Hazard, alisajiliwa na klabu ya Chelsea mwaka 2012 akitokea nchini Ufaransa akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Lille ambayo kwa mwaka huo ilikuwa bingwa wa Ligue 1