Herrera Akubali Chicharito Kucheza Soka Real Madrid

Kocha wa timu ya taifa ya Mexico Miguel ‘Piojo’ Herrera amembashiria mema mshambuliaji kutoka nchini humo Javier Hernández Balcázar Chicharito, baada ya kujiunga na klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid kwa mkopo wakati wa usajili wa majira kiangazi.

Herrera, amebashiri kwamba Chicharito, atakuwa na kiwango cha hali ya juu tofauti an alivyokuwa Man utd, kutokana na mfumo mzuri unaotumiwa na meneja wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti ambao haumbagui mchezaji yoyote klabuni hapo.
Herrera, amethibitisha kuwa na uhakika wa kumuona Chicharito akiwa katika kiwango tofauti wakati akihojiwa na kituo cha televisheni cha Sports TV mwishoni mwa juma lililopita.
Amesema ni wakati mzuri sana kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, kuonyesha uwezo wake na hana shaka na kile kitakachotokea baada ya miezi michache akiwa na kikosi cha Real Madrid ambacho kimeshuhudia Chicharito akifunga mabao mawili katika michezo mitatu aliyocheza mpaka sasa.
Katika hatua nyingine kocha huyo aliekiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Mexico hadi katika hatua ya 16 bora wakati wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 kule nchini Brazil, amekiri aliufuatilia mchezo wa Real Madrid wa mwishoni mwa juma lililopita ambapo walicheza dhidi ya Deportivo ambao walikubali kichapo cha mabao manane kwa mawili.
Amesema katika mchezo huo Chicharito, alicheza katika kiwango cha juu na hatiame kufanikiwa kufunga mabao mawili kwa ufundi mkubwa kutokana na mashuti makali aliyoyaelekeza langoni mwa wapinzani.
Javier Hernández Balcázar Chicharito, alilazimika kupelekwa kwa mkopo Real Madrid akitokea Man Utd, baada ya kushindwa kumridhisha meneja Louis van Gaal wakati wa maandilizi ya msimu wa 2014-15.

Popular Posts