Jay Z ashitakiwa kwa kuimba kionjo cha wimbo 'Run This Town', naye ajibu tuhuma
Rapper Jay Z anakabiliwa na kesi akituhumiwa kusample bila
kibali kionjo cha wimbo wa mwaka 1969 na kukitumia kwenye wimbo wake Run
This Town wa mwaka 2009.
Record label ya TufAmerica imetangaza kuwa inamshitaki Jay Z kwa
kusampe ‘Oh’, sio sentensi wala neno, ile “Oh” inayosikika kwenye Run
Town. Record label hiyo inadai aliisample bila ruhusa kutoka kwenye
wimbo Eddie Bo wa mwaka 1969 ‘Hook and Sling’.Hata hivyo, Jay Z aliamua kujibu kupitia mwanasheria wake ambaye alikanusha tuhuma hizo na kudai kuwa hakukuwa na mantiki ya kiubora wala kiukubwa kuwa alisampo syllable hiyo.
“Even if one short word – or the recording thereof – could possibly be deemed original enough to warrant copyright protection, this fleeting and generic phrase is neither quantitatively nor qualitatively significant.”
