ligi ya mabingwa Ulaya
Katika
michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya leo kuna kivumbi kingine ambapo
CSKA Moscow itakuwa na kibarua kigumu pale watakapowakaribisha Bayern
Munich.
Wakati huo huo Man City waliopigwa bao moja na Bayern Munich watakutana na AC Roma iliyowapiga CSKA Moscow mabao matano katika mechi iliyopita.
Paris St G ya Ufaransa wao wanakutana uso kwa uso na Barcelona
Ukumbumbuke katika mechi ya wikendi iliyopita Paris St G walitoka sare na Ajax bao moja kwa moja.
Ajax inakutana leo na Apoel Nic ambayo ilipigwa na Barcelona bao moja katika mechi ya awali.
Sporting Lisbon ya Ureno leo wanapepetena na Chelsea ya England. Meneja Jose Mourinyo amesema kutokana na umuhimu wa mechi hii atajitoa muhanga kwa kumchezesha mshambuliaji machachari Diego Costa.
Schalke waliotoka moja moja na Chelsea wanacheza na NK Maribor ambayo wiki iliyopita ilitoana jasho na Sporting Lisbon kiasi cha kutoka na bao moja kwa moja.
BATE Bor itakipiga na Ath Bilbao
Shakt Donsk inashuka dimbani dhidi ya FC Porto iliyowachapa mabao sita BATE Bor
Mechi kamili za leo hizi hapa
- CSKA v Bayern Munich
- City v Roma
- Paris St G v Barcelona
- Sporting v Chelsea
- Apoel Nic v Ajax
- Schalke v NK Maribor
- BATE Bor v Ath Bilbao
- Shakt Donsk v FC Porto