Madaktari Wamshawishi Li Na Kuachana Na Racket
Bingwa mara mbili wa mataji makubwa katika mchezo wa tennis,
Li Na ametangaza kustaafu mchezo huo kwa shinikizo la majeraha
yanayomkabili.
Li Na, ambaye ni raia wa nchini China amelazimika
kufanya hivyo baada ya kuthibitishiwa na daktari wake, taarifa za kutorejea katika hali yake ya kawaida kufuatia majeraha ya mara kwa mara yanayomuandama.
Li Na, mwenye umri wa miaka 32, ametangaza maamuzi hayo huku mashabiki wa mchezo wa tennis wakikumbuka kumuona kwa mara ya mwisho akiwa uwanjani wakati wa michuano ya Wimbledon iliyofanyika mwezi Juni mwaka huu nchini Uingereza.
Mwanadada huyo ameondoka kwenye mchezo wa tennis baada ya kutwaa taji la Australian Open mwezi Januari mwaka huu, likitanguliwa na taji la French Open mwaka 2011 ambapo alijiwekea mkazo wa kufahamika duniani kote.
Li Na, naondoka katika viwanja vya tennis akiwa katika nafasi ya sita katika orodha ya viwango vya ubora wa mchezo huo duniani upande wa wanawake.

Pia alikuwa mwanamichezo wa kwanza kupeleka taji kubwa la michuno ya tennis barani Asia baada ya kufanya hivyo mwaka 2011 kwa kumuangusha nguli kutoka nchini Urusi Maria Sharapova katika mchezo wa hatua ya fainali ya michuano ya Australian Open.