Magaidi wa Algeria wamchinja mtalii kutoka Ufaransa kuiunga mkono ISIS

Kundi la kigaidi la Jund al-Khilifa limemuua kwa kumchinja mtalii wa Ufaransa ikiwa ni sehemu ya ahadi yao kwa nchi hiyo ikiwa haitasitisha mashambulizi dhidi ya kundi la ISIS nchini Iraq.

Jumapili iliyopita,  kundi hilo liliweka YouTube video inayoonesha wapiganaji walijifunga kitambaa usoni wakimfanyia tukio hilo mtalii aliyetajwa kwa jina la Herve Gourdel mwenye umri wa miaka 55, waliyemteka alipokuwa nchini humo.
Ufaransa imeungana na Marekani katika kampeni ya kushambulia kundi la ISIS lililoteka sehemu kubwa nchini Iraq na Syria.

Popular Posts