Mapenzi: Hii ndio adhabu bora zaidi inayopendekezwa unapomfumania mpenzi wako
Moja kati ya nyakati ambazo akili hutakiwa kufanya kazi kwa
kiwango kikubwa zaidi ili kuchukua uamuzi sahihi ni wakati ambapo moyo
umevunjika vipande vyote baada ya kumfuma mwizi wa tunda lako la moyo
akilila kama lake.
Fumanizi huupasua moyo na kuumiza misuli yote ya mwili kiasi cha kupampu kwa nguvu zote sumu ya hasira iliyo mwilini mwako. Lakini huu ndio wakati ambapo ukizifuata hisia zako unaweza kufanya maamuzi ambayo utayajutia maisha yako yote pindi hasira hizo zitakapozimika.
“Japo naweza kuonekana kama nina kichaa vile, lakini ukweli ni kwamba njia bora ya kumu adabisha mpenzi wako anaekusaliti ni kumpenda zaidi badala ya kumdhuru au kujidhuru wewe mwenyewe.”Amesema Amani Misana kwenye maelezo yake.
“Kumbuka aina yoyote ile ya kudhuru madhara yake ni lazima yarudi kwako kwa njia moja ama nyingine lakini pia uliyempenda kwa ukweli huwezi kumdhuru kwani falsafa ya upendo wa kweli inasema pendaneni kwa wema hata kama mtaachana basi achaneni kwa wema. Kwa kuwa mapenzi ni wema.” Ameongeza.