Marekani yatoa video inayoonesha mashambulizi ya anga dhidi ya ISIS nchini Syria

Makao Makuu ya Ulinzi, Pentagon Marekani imetoa kipande cha video inayoonesha jinsi walivyotekeleza na kufanikisha mashambulizi ya kwanza nchini Syria dhidi ya kundi linalojiita Islamic State Of Syria and Iraq (ISIS).

September 23 jeshi la Marekani lilitekeleza mashambulizi ya anga katika makao makuu ya kundi hilo Ar Raqqah, Syria.
Marekani na washirika wake wamelenga kushambulia na kutokomeza kundi hilo linalotekeleza mauaji na kuwachinja raia wa Marekani na Uingereza huku wakionesha katika vipande vya video.

Popular Posts