Martinez Awatuliza Mashabiki Waliochukizwa Na Kiwango Cha Tim Howard
Baada ya mashabiki wa klabu ya Evrton kuendelea kumzonga
mlinda mlango wa klabu hiyo Tim Howard, kwa kumshutumu alicheza chini ya
kiwango wakati wa mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya
Crystal Palace, Roberto Martinez amekuwa mtu wa kwanza kukinga kifua.
Martinez, amejitoa muhanga kama meneja wa kikosi cha Everton na kuwataka mashabiki kuacha utaratibu wa kumzonga mlinda mlango huyo na badala yake amewahimiza kusamehe na kuangalia mbele.
Martinez, amesema kila shabiki wa klabu hiyo ana haki ya kusema chochote ambacho kimemgusa lakini anaamini muda wa kumzonga Howard umeshapita na kilichobaki ni kuendelea kuwa pamoja kwa ajili ya kuhakikisha michezo inayofuata wanarekebisha makosa na hatimae kuondoka na ushindi.
Amesema amefuatilia kwa ukaribu mzozo uliokuwa unaendelea baina ya mashabiki waliokuwa wanamtetea Howard dhidi ya wale waliomponda kutokana na kiwango chake wakati wa mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita na ameumizwa sana na lawama ambazo zimepelekwa kwa kipa huyo kutoka nchini Marekani.
"Hakuna haja ya kuendelea kulumbana, mashabiki wanatakiwa kutambua kwamba wachezaji wanahitaji msaada wao na siku zote mambo yanapoharibika hakuna wigo wa kulaumiana kupita kiasi, kama ilivyo kwa Howard.” Amesema Martinez.
“Ni kweli tumepoteza mchezo nyumbani kwa kufungwa mabao matatu na Crystal Palace na kila mmoja wetu ameumizwa na matokeo hayo kutokana na uhalisia wa mapenzi tuliyonayo dhidi ya Everton, lakini naamini michezo ipo mingi kuna haja ya kila mmoja kumuamini mwingine ili kupisha mikakati ya kujipanga vizuri kwa ajili ya kusaka point tatu mbele ya safari.” Ameongeza Martinez.
Asilimia kubwa ya mashabiki wa Everton walikuwa wanahoji kiwango cha Tim Howard, kwa kulinganisha na uwezo mkubwa aliouonyesha wakati wa fainali za kombe la dunia kwa kuisaidia timu yake ya taifa ya Marekani ambayo ilifika hatua ya 16 kwa msaada wake.