Martinus Ignatius "Mart" Nooij Ataja Watakaoivaa Benin

Wachezaji 26 wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kwa ajili mchezo wa Kalenda ya Shirikisho la soka duniani FIFA dhidi ya timu ya taifa ya Benin (The Squirrels) utakaochezwa Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam
.
Kocha Mart Nooij ambaye yuko Cairo, Misri kwenye kongamano la makocha la Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), amesema kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kitaingia kambini Oktoba 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Wachezaji walioitwa ni makipa Deogratias Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam), na Mwadini Ali (Azam).
Mabeki ni Said Moradi (Azam), Shomari Kapombe (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Miraji Adam (Simba), Charles Edward (Yanga) na Emmanuel Simwanda (African Lyon).
Viungo ni Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba) na Haruna Chanongo (Simba).
Washambuliaji ni Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City), na Juma Liuzio (Zesco, Zambia).

Popular Posts